HALMASHAURI YA WILAYA YA BAHI YAHAMASISHA WANANCHI WAKE KUJIUNGA NA MFUKO BIMA YA AFYA YA JAMII (CHF ILIYOBORESHWA).
Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi wakishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Bahi (Bibi.Rachel Chuwa) wameamua kulivalia njuga suala la Afya Bora kwa Wananchi wake baada kupita katika Vijij vyake vyote Hamsini na Tisa (59) kuhamasisha na kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kutumia huduma nafuu za Bima ya Afya ya CHF-ILIYOBORESHWA.
Aidha, Zoezi hilo la Uhamasishaji liliungwa Mkono kwa nguvu zote na Mkuu wa Wilaya ya Bahi MH. ELIZABETH KITUNDU ambaye aliambatana na timu ya Uhamasishaji kutilia mkazo kwa Wananchi juu umuhimu wa kujiunga na Bima ya afya pamoja na kutoa Matangazo mengine ya Kiserikali kama vile Ujenzi wa Vyoo,Utanzaji wa Chakula,Upigaji Chapa Ng’ombe ,Usafi wa Mazingira na Udumishaji wa Amani.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa